Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili aing’ang’ania Chadema 
Habari za Siasa

Msajili aing’ang’ania Chadema 

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imetoa siku sita kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwasilisha ratiba ya mkutano mkuu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sisty Nyahozi, kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Chadema inatakiwa kuwasilisha ratiba hiyo kabla ya tarehe 11 Novemba 2019.

“Taarifa hiyo iwasilishwe Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, siyo zaidi ya tarehe 11 Novemba 2019, saa tisa na nusu mchana,” inaeleza taarifa hiyo.

Ofisi hiyo imeitaka ratiba ya Chadema ioneshe tarehe ya utoaji fomu za kugombea, uteuzi na uchaguzi wa wanachama wenye nia ya kugombea.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Chadema kinapaswa kuwasilisha ratiba hiyo ili kurahisisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake.

“Ofisi ina mamlaka ya kufuatilia uchaguzi na uteuzi wa viongozi wa vyama vya siasa, ili kuhakikisha unafanyika kwa mujibu wa sheria,” imeeleza taarifa hiyo.

Ofisi hiyo ya msajili, tarehe 1 Oktoba 2019 iliiandikia barua Chadema ili kueleza sabababu za kutofanya uchaguzi wa viongozi wa chama, na kukipa siku siku kujibu barua hiyo.

Barua hiyo ilieleza kuwa, Chadema kimevunja sheria kwa kutoitisha mkutano mkuu pamoja na kutofanya uchaguzi wa viongozi wapya, licha ya kipindi cha uongozi wa viongozi wake kikatiba kuisha.

Sehemu ya barua hiyo ilieleza kwamba, Chadema kinapaswa kuwasilisha maelezo yake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kwanini kisichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba na Kanuni za hicho.

Barua hiyo ya msajili iliitaka Chadema kuwasilisha maelezo yake ndani ya siku saba, ambapo mwisho ilikuwa leo saa 9.30 mchana.

Tarehe 7 Oktoba 2019, Dk. Vincent Mashinji  ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliandika barua ya kujibu, kwamba waliandika tarehe maalum ya kufanya uchaguzi hup.

“Tumepeleka barua ya majibu asubuhi ya leo (tarehe 7 Oktoba 2019). Ratiba yetu iko pale pale, tarehe 18 Desemba 2019 tutafanya uchaguzi wa viongozi,” alisema Dk. Mashinji.

Hata hivyo, msajili anaitaka Chadema kuwasilisha ratiba ya uchaguzi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!