Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msaidizi wa Sabaya aanza kutoa ushahidi kesi ya Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Msaidizi wa Sabaya aanza kutoa ushahidi kesi ya Mbowe

Spread the love

 

JUSTIN Elia Kaaya, aliyekuwa mfanyakazi wa Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, ameanza kutoa ushahidi wake katika kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Kaaya ambaye ni shahidi wa pili wa Jamhuri, ameanza kutoa ushahidi wake leo Jumatano, tarehe 27 Oktoba 2021, mahakamani hapo akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Akiongozwa na Wakili Chavula, Kaaya amedai alianza kufanya kazi kwa Sabaya mwaka 2017 kama mpiga picha hadi 2018 alipoteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Kilimanjaro alipokuwa msaidizi wake, ikiwemo kumpelekea chakula ofisini kwake.

Kaaya amedai kuwa, Oktoba 2018 aliondoka nyumbani kwa Sabaya alikokuwa anaishi naye mkoani Kilimanjaro na kurudi nyumbani kwake Longido mkoani Arusha.

Shahidi huyo wa Jamhuri amedai, Novemba 2018 alipokea simu kutoka kwa Mbowe akimtaka waonane lakini alisitia kwa kuwa alikuwa na hofu kwani hakuwa na mahusiano naye kabla.

Kaaya amedai, baada ya kusita Mbowe aliamua kumfuata mwenyewe mkoani Arusha, ambapo walionana majira ya saa tatu usiku ndani ya uwanja wa mpira uliko mji Mdogo wa Longido, na kuingia katika gari yake.

Kaaya amedai, baada ya kuingia ndani ya gari, Mbowe alimwambia Ole Sabaya anamsumbua sana pale Hai na kuwa yeye ni mtu wake wa karibu, na kumtaka ampe taarufa za shughuli anazofanya na watu aliokuwa nao.

Amedai, Mbowe alimuambia kuwa yeye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinxani hivyo atafanya namna yoyote anavyoweza kumrudisha kwa sabaya ambapo amesema alimjibu akisema hawezi kwa kuwa aliamua kufanya shughuli xake binafsi.

Kaaya amedai, baada ya kutoa kauli hiyo, Mbowe alimpa Sh.300,000 akisema ni za usmbufu na kwamba baada ya hapo waliagana akaondoka.

Amedai baada ya Mbowe kuondoka alimpigia simu sabaya ili ampe taarifa lakini hakupokea simu. Ndipo akampigia simu Mbunge wa Longido, Dk Steven Kiruswa kumueleza kilichotokea.

Kaaya amedai, mwanzoni mwa 2020 Mbowe alimpigia simu kwa mtandao wa Whatsapp, akimtaka waonane amfuate Moshi kwa kuwa yeye alikuwa Arusha.

Akiongozwa na Wakili Chavula, Kaaya amedai baada ya wito huo alipanda usafiri wa Costa kuelekea Moshi.

Sehemu ya mahojiano yako hivi;

Shahidi: Akasema tumepotezana sana chief.

Wakili wa Serikali: Alikupa ujumbe gani?

Shahidi: Akasema anataka tuonane.

Wakili wa Serikali: Wapi?

Shahidi: Moshi. Wakati huo nilikuwa Arusha.

Wakili wa Serikali: Wewe ukasemaje?

Shahidi: Ngoja nimalizie kumwagilizia shambani huku nikishamaliza nitakuja.

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea kutokana na ahadi yenu?

Shahidi: Baada ya kumalizia shughuli zangu nilipanda Coaster na kumpigia simu kwamba naenda.

Wakili wa Serikali: Ulipanda Coaster kuelekea wapi?

Shahidi: Moshi Kilimanjaro.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulifika hadi wapi?

Shahidi: Baada ya kumpa taarifa kuwa nipo kwenye gari akasema nishuke Machame Road.

Wakili wa Serikali: Kwa namba ipi?

Shahidi: Ileile ya 0784-779 944.

Wakili wa Serikali: Ulipomueleza akakupa maelekezo yapi?

Shahidi: Akaniambia nishuke Machame Road.

Wakili wa Serikali: Ipo wapi?

Shahidi: Ipo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wakili wa Serikali: Tueleze sasa baada ya kupewa maelekezo hayo nini kilitokea?

Shahidi: Nilishuka kwenye gari nikapiga tena simu.

Wakili wa Serikali: Simu ipi?

Shahidi: Namba yake ile ile ya 0784-779 944.

Wakili wa Serikali: Ulipompigia simu nini kilitokea?

Shahidi: Akaniambia nisubiri hapo nakuja.

Wakili wa Serikali: Nini kilijiri?

Shahidi: Baada ya muda akinipigia simu kuniambia umefika umekaa upande upi? Akaniambia vuka, kaa upande wa kulia.

Wakili wa Serikali: Wewe ulikutana na nini?

Shahidi: Palikuwa na barabara ya kwenda Machame na nyingine kwenye Arusha na nyingine Moshi.

Wakili wa Serikali: Nini kikatokea?

Shahidi: Ilikuja gari aina ya Land Cruiser V8 yenye mlingoni na bendera ya bunge ikiwa na plate namba zilizoandikwa KUB.

Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?

Shahidi: Ilisimama upande wangu. Ikashusha kioo upande wa abiria. Nikamwona Mwenyekiti akaniambia panda.

Wakili wa Serikali: Baada ya kuambiwa upande nini kilitokea?

Shahidi: Alishuka mtu kutoka siti ya nyuma akaniambia “pita”. Nikaingia kwenye gari.

Wakili wa Serikali: Eheee!

Shahidi: Ile gari ilienda mwelekeo wa kwenda Machame. Baadae tukaingia sehemu ambayo nilikuja kugundua ni Hotel ya Aishi.

Wakili wa Serikali: Palikuwa na watu gani kwenye gari?

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!