August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msafara wa Lowassa wazuiwa

Spread the love

MSAFARA wa Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umezuiwa kuingia Mkoa wa Rukwa na Katavi, anaandika Faki Sosi.

Lowassa amezuiwa na Jeshi la Polisi kwa madai kuwa, msafara wake unaweza kuingilia ziara inayofanywa na Majaliwa kwenye mikoa hiyo.

Lowassa ambaye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana aliungwa mkono na Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha NCCR-Mageuzi na NLD, juzi alikuwa mkoani Songwe ambapo alikutana na viongozi wa chama hicho katika mkutano wa ndani.

Frank Mwaisumbe, Katibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, ameeleza kuwa Lowassa alipigiwa simu akiwa Tunduma na kupewa taarifa ya kuzuiwa.

George Kyando, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa amesema, waliwashauri Chadema kubadili ratiba kutokana na ziara ya Majaliwa.

error: Content is protected !!