Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Ndugai: Balozi Kagasheki amtumia ujumbe Rais Samia
Habari za Siasa

Mrithi wa Ndugai: Balozi Kagasheki amtumia ujumbe Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM
Spread the love

 

WAZIRI wa zamani wa maliasili na utalii nchini Tanzania, Balozi Khamis Kagasheki amemwomba Mwenyekiti wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan kuwatafutia spika mwenye sifa za nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Balozi Kagasheki aliyewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, mkoani Kagera ametoa nahasa hizo asubuhi ya leo Alhamisi, tarehe 20 Januari 2022, ikiwa ni saa chache kabla ya Rais Samia kuongoza kikao cha kamati kuu.

           Soma zaidi:-

Lengo la kikao hicho, kinachofanyikia makao makuu ya CCM ‘White House’ jijini Dodoma ni kuchunja na kuteua wagombea uspika watakaomrithi Job Ndugai aliyejizulu tarehe 6 Januari 2022.

Jumla ya wagombea 70 wamejitokeza kwenye mbio hizo za kuwania uongozi wa muhimili wa Bunge wakiwemo wanasheria, wasanii, wabunge wa sasa na wa zamani, wasomi na wanachama wa kawaida.

Kikao hicho cha leo, kitateua majina ya wanachama watatu watakaokwenda kupigiwa kura na kamati ya wabunge wa CCM kisha kupata jina moja litakalokwenda kushindanishwa bungeni na wagombea wa vyama vingine.

Balozi Kagasheki ametumia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuandika “Mwenyekiti wetu, Mhe @SuluhuSamia katika vikao vya Chama chetu tunaomba mtutafutie Speaker wa Bunge mwenye sifa za nafasi hiyo.”

Ameongeza, “ajue Katiba ya nchi, azijue kanuni na taratibu za Bunge, muamuzi makini wa mijadala,, mwenye heshima, sio mropokaji, mwenye maono.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!