September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrithi wa Manji kupatikana Januari

Jengo la Yanga

Spread the love

BAADA ya sintofahamu ya muda mrefu hatimaye Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Malangwe Mchungahela imetangaza 13 Januari, 2019 kuwa ndiyo tarehe ya uchaguzi ndani ya klabu ya Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Uchaguzi huo ambao utafanyika katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji, ambao wote walijiudhulu nafasi zao ndani ya klabu hiyo katika vipindi tofauti.

Yanga wanaingia katika uchaguzi huo baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kutaka uongozi wa klabu hiyo kutangaza tarehe ya Uchaguzi kwa ajiri ya kuziba nafasi za waliojiuzuru nafasi zao kama katiba yao inavyosema.

Kwa mantiki hiyo Yanga inakwenda katika uchaguzi huu huku swala la wanachama wa klabu hiyo kumtaka aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji kurudi ndani ya timu hiyo kama walivyo afikiana kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika 10 Juni, 2018 kugonga mwamba.

error: Content is protected !!