August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrithi wa Makonda atoa onyo

Spread the love

ALI Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka wafanyabiashara kutoijaribu serikali kwa kupandisha bei za bidhaa hasa katika kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, anaandika Happiness Lidwino.

Hapi ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano lililokutanisha taasisi za kiislamu 100, kujadili athari za ukuaji wa teknolojia katika mawasiliano.

“Wapo wafanyabiashara wenye nia ya kuikomoa serikali kwa kutaka kuilazimisha kuagiza bidhaa za nje, msitumie mwezi wa ramadhani kuficha vyakula, serikali haitawaangalia tutadhibiti bei za bidhaa,” amesema.

Akizungumzia athari za teknolojia Hapi amesema, “teknolojia ndiyo kiini cha maendeleo na kubainisha kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa maadili. Semina iwekewe mkakati endelevu hasa wakati huu tunapopokea teknolojia kila siku,”amesema.

Aidha Hapi amelaani mauaji yaliyotokea mjini Mwanza na kubainisha kuwa suluhu ya migogoro si kuchinja watu na kusisitiza amani sanjari na kumuombea rais Dk John Magufuli katika utendaji kazi wake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Semina hiyo, Shekh Abdallah Ndauga amesema, ukuaji wa teknolojia umekuja sura chanya yenye maendeleo na sura hasi kwa kutumika katika vitendo viovu kama uhalifu na uvunjifu wa amani sambamba na mmomonyoko wa maadili.

“Viongozi wa dini hawapaswi kuwahubiria waumini kwenye nyumba za ibada wafanye semina kama hizi, hasa kwa vijana kama ambavyo taasisi yetu yenye lengo la kutoa elimu uelewa na stadi za mawasiliano kwa madhumuni ya ustawi wa jamii,”amesema.

Aidha Sheihk Waziri Maduga, amewaasa waumini hao kuitumia teknolojia katika maadili”Tukisema teknolojia ni muhimu isiwe na kikwazo katika dini itusaidie zaidi ni wajibu wetu kujifunza kwasababu yana msingi,” amesema.

error: Content is protected !!