July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrithi wa Maalim Seif ACT-Wazalendo kupatikana Novemba 27

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

 

KAMATI Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, imeagiza mkutano wa dharura wa chama hicho uitishwe tarehe 27 Novemba 2021, kwa ajili ya kujaza nafasi ya Mwenyekiti wake Taifa, iliyoachwa wazi na Hayati, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia tarehe 17 Februari mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, tarehe 20 Juni 2021 na Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa ACT-Wazalendo, Salim Bimani, akitangaza maazimio ya kikao cha kamati hiyo, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Kamati Kuu ilijadili masuala mbalimbali ya kichama na kitaifa na kutoka na maazimio, ikiwemo kuazimia mkutano mkuu wa chama wa dharura uitishwe tarehe 27 Novemba 2021, kwa ajili ya kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa,” imesema taarufa ya Bimani.

Taarifa ya Bimani imeongeza “iliyoachwa wazi baada ya kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad.”

Taarifa ya Bimani imesema, ratiba ya uchaguzi wa mwenyekiti huyo itatangazwa baada ya kuidhinishwa na Halmashauri Kuu ya ACT-Wazalendo Taifa.

Maalim Seif aliyezikwa kijijini kwao Nyali Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar, tarehe 18 Februari 2021, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Machi 2020. Aliitumikia nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja, hadi umauti ulipomkuta.

error: Content is protected !!