Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Khatib katika Jimbo la Konde kupatikana leo
Habari za SiasaTangulizi

Mrithi wa Khatib katika Jimbo la Konde kupatikana leo

Spread the love

 

WANANCHI wa Jimbo la Konde, Visiwani Zanzibar, leo Jumapili tarehe 18 Julai 2021, wanachagua mbunge wao, ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Khatib Said Haji, aliyefariki dunia tarehe 20 Mei mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Haji aliyekuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu. Mwili wake ulizikwa siku hiyo hiyo nyumbani kwao Pemba, Zanzibar.

Kufuatia kifo hicho, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), iliitisha uchaguzi huo mdogo, ambapo vyama 12 vimejitosa kulisaka jimbo hilo.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo,vinachuana vikali kulitwaa jimbo hilo.

ACT-Wazalendo kimemteua Mohammed Said Issa, kulitetea jimbo hilo lililokuwa linashikiliwa na mwanachama wake Khatib, aliyefariki dunia. Huku CCM kikimteua Sheha Mpemba Faki, kugombea jimbo hilo.

Khatib aliliongoza Jimbo la Konde kwa muda wa miaka 10 mfululizo, kupitia Chama cha Wananchi (CUF).Kuanzia 2010 hadi 2020.

2020 alihamia ACT-Wazalendo na kugombea jimbo hilo. Aliliongoza jimbo hilo kupitia chama hicho kwa muda wa miezi mitano, kuanzia tarehe 15 Disemba 2020, alipoapishwa kuwa Mbunge na Spika Job Ndugai, hadi alipofariki dunia Mei 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!