May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrithi wa Dk. Mpango Buhigwe kupatikana 16 Mei

Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania akiapa mbele ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma

Spread the love

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza tarehe 16 Mei 2021, kufanyika kwa uchaguzi mdogo jimbo la Buhigwe, mkoani Kigoma na kata 18. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya aliyekuwa mbunge wake, Dk. Philip Mpango, kuteuliwa tarehe 30 Machi 2021, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Jina la Dk. Mpango, liliwasilishwa bungeni siku hiyo kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge ambapo wabunge 363 waliohudhuria kikao, walimkubali sawa na asilimia 100.

Siku hiyohiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliitarifu Tume ya Uchaguzi kuanza taratibu za uchaguzi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Mpango ambaye tarehe 31 Aprili 2021, aliapishwa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

Leo Ijumaa, tarehe 9 Aprili 2021, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera amesema, fomu za ubunge wa Buhigwe na Udiwani kwenye kata hizo 18 zitaanza kutolewa, 24 hadi 30 Aprili 2021.

Uteuzi wa wagombea utafanyika 30 Aprili 2021 na kesho yake yaani 1 hadi 15 Mei 2021 ni kampeni na kesho yake 16 Mei 2021 ni siku ya uchaguzi.

Msingi wa Jimbo hilo kuwa waz ni, Dk. Mpango aliyeuliwa na Rais Samia kushika wadhifa huo ili kujaza nafasi ya Samia aliyekuwa makamu wa Rais ambaye tarehe 19 Machi 2021, aliapishwa kuwa Rais.

Samia aliapishwa kuwa Rais baada ya aliyekuwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, kufariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mwili wa Dk. Magufuli, ulizikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita tarehe 26 Machi 2021.

error: Content is protected !!