Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Dk. Bashiru aeleza alivyopokea taarifa za uteuzi
Habari za Siasa

Mrithi wa Dk. Bashiru aeleza alivyopokea taarifa za uteuzi

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Kiongozi wa Tanzania, Balozi Hussein Athuman Kattanga, amesema, taarifa za uteuzi wa nafasi hiyo, alizipata akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akielekea Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema hayo leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Balozi Kattanga aliteuliwa kushika wadhifa huo jana Jumatano tarehe 31 Machi 2021 na Rais Samia, akichukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally, aliyeteuliwa kuwa mbunge.

Akielezea namna alivyopata taarifa hizo, Balozi Kattanga amesema, jana mchana alichukuliwa na maafisa wa serikali kwa kushtukizwa, ambao waliomueleza anatakiwa aende Dodoma, pasipo kumwambia anakwenda kufanya nini.

Katibu Mkuu kiongozi huyo amesema, taarifa hizo alizipata akiwa katika maandalizi ya kurudi katika kituo chake cha kazi, Ubalozi wa Japani, na kwamba alilazimika kughairisha safari kwani alikuwa ameshakata tiketi ya ndege.

“Leo nilikuwa nirudi Japan kwa maelekezo ya katibu mkuu wizara ya mambo ya nje na tiketi ile ya Japan ikabidi niighairishe sababu jana majira ya saa sita hivi, nikachukuliwa naambiwa fuata huku ongoza huku Airport (uwanja wa ndege),” amesema Balozi Kattanga.

Balozi Kattanga amesimulia “nikaambiwa chukua tiketi, mambo mengine utajua huku Dodoma, bahati nzuri nilipokuwa uwanja wa ndege nikawa naangalia TV ndio nikajua kabla sijafika Dodoma.”

Akitaja vipaumbele vyake katika majukumu yake mapya, Balozi Kattanga amesema, atakuwa kiungo mzuri kati ya Serikali na taasisi zake.

“Jambo muhimu, kazi ya katibu mkuu kiongozi ni ku-coordinate (kuratibu) sababu serikali kwa mujibu wa taratibu huwa inakatwa vipande vipande, wizara na taasisi zake kwa hiyo, kazi ya katibu mkuu na ofisi ya waziri mkuu kui-cordinate (ratibu) serikali isifanye kazi tofauti,” amesema Balozi Kattanga.

Amesema “hizi wizara na taasisi zake zimewekwa ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa kazi na taaluma, inapofika serikali inayotaka kufika dira ya 2025 lazima iwe serikali inayofanya kazi pamoja.”

Balozi Kattanga amesema katika utekelezaji wa majukumu yake, atahakikisha Serikali inafanya kazi kwa ufanisi kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

“Leo tuna wizara zipo kadhaa na ndani yake kuna taasisi kadhaa lakini kazi ya baraza na kikao cha makatibu wakuu, ku-cordinate serikali kwenda kwenye barabara ya kufika 2025, maana yake serikali inatakiwa iwe effective and efficiency for deliver (iwe fanisi kwa ajili ya kupata matokeo yenye ufanisi),” amesema Balozi Kattanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!