January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrema, Selasini wamkomalia Gama

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (kushoto) akiwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema

Spread the love

WABUNGE Joseph Selasini (Rombo) Chadema na Augustino Mrema (Vunjo) TLP, wameendelea kumtaka Rais Jakaya Kikwete, kumwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ndani ya siku saba kutokana na kutumia madaraka yake vibaya. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Wabunge hao kwa pamoja leo wameitisha mkutano na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge wakisema kuwa kiongozi huyo wa mkoa amekuwa ni dalali asiyefanya kazi yoyote zaidi ya kuuza mashamba ya watu.

Awali kabla ya mkutano huo, Mrema aliomba mwongozo wa Spika bungeni kwa jambo hilo hilo lakini, Spika wa Bunge Anne Makinda, akaagiza Wizara husika kufanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti kabla ya Bunge halijavunjwa ili ukweli ujulikane.

Mwanzoni mwa wik,i Msemaji wa kambi ya upinzani bungeni kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee, alimtuhumu Gama kuwa ametumia madaraka yake kwa kumuingiza mwanawe katika mradi wa uporaji wa ardhi kwa wananchi.

Hata hivyo, juzi akiwa mkoani Kilimajaro, Gama alikanusha tuhuma hizo akisema ni masuala ya kisiasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo alitaka wananchi kuyapuuza.

Lakini leo, Selasini amesema kuwa Gama wakati akisafiri nje ya nchi, alitumia fedha za umma wakati uchunguzi ulibaini kuwa alikuwa anakwenda kwa maslahi yake binafsi.

“Hii ni dhahiri kwa kuwa mtoto wake tayari alikuwa mbia katika kampuni hiyo na ni dhahiri kwamba mtoto huyo ndiye aliyewashawishi washirika wake waje kuwekeza Tanzania,” amesema Selasini.

Mbunge huyo aliomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imchunguze Gama sambamba na watendaji wa Serikali waliotumia madaraka yao na kutumia fedha za umma kuanzisha kampuni binafsi.

Kingine ambacho alisisitiza ni kumtaka Mkuu huyo kurudisha kiasi cha Sh. 168 milioni za Halmashauri ya Rombo kwa kuwa zilitumika kufanya shughuli binafsi na wananchi pamoja na halmashauri hawakunufaika.

Kwa upande wake, Mrema amesema kuwa ataungana na wananchi kuhakikisha Mkuu wa mkoa anang’oka kwa kuwa ni mchwa usiobebeka.

Mrema amesema kuwa Gama alijimegea ekari 2000 katika eneo la ekari 2470 lililobaki baada ya ekari zingine 140 kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa soko la kimataifa la Himo.

“Gama bila ya kushirikiana na wenzake, aliufuta Ushirika ambao ulikuwa ukimiliki eneo hilo tangu miaka ya 1960 na kuunda kampuni aliyoiita ni Kilimanjaro Uchumi Cooperative Ltd.

error: Content is protected !!