MKURUGENZI wa Itifaki na Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania John Mrema amesema, “mimi ni mzima wa afya.” Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Mrema ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 10 Machi 2021, alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online, baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba amefariki dunia.
Katika mazungumzo yake, Mrema amesema “mimi ni mzima wa afya, naendelea na majukumu yangu na hizo taarifa kuwa nimefariki sijui wanazitoa wapi.”
“Nipo nyumbani naendelea na kujikinga na corona,” amesema Mrema huku akitoa tahadhari kwa wananchi kujikinga na ugonjwa huo.
Leave a comment