August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrema: Mfikishieni ushauri huu Magufuli

Spread the love

AUGUSTINO Mrema, Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) amesema, ushauri wake kwa Rais John Magufuli ni kubadili mwelekeo wake kwa vyombo vya habari, anaandika Josephat Isango.

Amesema, Rais Magufuli ili afanikiwe kwenye vita ya kutumbua majipu anayokabiliana nayo, anapaswa kujenga urafiki na vyombo vya habari.

Mrema amesema hayo leo alipozungumza na mtandao huu alipopiga simu kupongeza gazeti la MwanaHalisi kwa habari zake za uchunguzi kuhusu ufisadi inazoripoti.

“Nimepiga simu leo kuwapongeza. Mnaandika habari za hatari lakini za kweli kwenye jamii, zinaonesha dhana ya utawala bora katika nchi yetu ilivyokuwa inaanza kufa na kwa serikali hii ya Magufuli, nadhani mtafanya kazi vizuri kwani anachukia ufisadi na mafisadi,” anasema Mrema na kuongeza;

“Nipo huku Kiraracha, Moshi Vijijini lakini kuna vijana wangu wameniletea gazeti hapa, naona mmeandika kuhusu utawala bora, hili limekuwa tatizo kwetu. Magufuli akiwaunga mkono, nchi hii itaenda mbele kama wakati ule nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.”

Mrema alirejea habari iliyoandikwa na Gazeti la MwanaHALISI kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa, imeogopa kuwafikisha mahakamani vigogo watano wa Wizara ya Fedha na Mipango iliyowataja katika waraka wake kwamba wanahusika na makosa ya rushwa na utakatishaji fedha.

Gazeti hilo limewataja wanaodaiwa kulindwa na serikali licha ya uhusika wao kwenye ukwapuaji huo ni Dk. Servasius Likwelile, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango; Ramadhani Kija, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha; Bedason Shalanda, Kamishna wa Uchambuzi wa Sera; Alfred Paul Misana, Kamishna Msaidizi Sera ya Madeni na Ngosha Said Magonya, Kamishna wa Fedha za Kigeni.

Majina ya vigogo hao yamo kwenye orodha ya wafanyakazi muhimu wa Wizara ya Fedha na Mipango na yaliorodheshwa na Takukuru katika mwasiliano yake kwenda kwa George Masaju, Mwanasheria ya Januari 20 mwaka huu.

error: Content is protected !!