July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrema ang’ang’ania TLP yake

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema akiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Nancy Mrikaria.

Spread the love

AUGUSTINE Lyatonga Mrema – Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), amesema hang’oki kwenye wadhifa huo licha ya baadhi ya watu kudai amechoka kiumri.Anaandika Pendo Omary….(endelea).

Badala yake, Mrema ameamua kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanywa na Mkutano Mkuu 23 Aprili 2015, katika Hoteli ya Kings Palace iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, akiwa ndiye mgombea pekee aliyechukua fomu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, amesema “mimi nina miaka 71. Rais wa Nigeria – Mohammadu Buhari aliyechaguliwa juzi-juzi ana miaka 72. Rais wa Zimbabwe – Robert Mugabe ana miaka 92. Mwenye umri mkubwa mnaniona mimi tu?”

“Kamati Kuu ya TLP iliyopita iliniteua kuongoza chama hiki. Pia wazee wa Vunjo wameniteua kuwania ubunge katika jimbo langu kwenye uchaguzi ujao. Ni kwa sababu wananiamini. Kwani hawakumuona mwingine? Amehoji Mrema.

Mkutano mkuu wa TLP utachagua viongozi wa ngazi mbalibali za kitaifa, likiwa ni agizo la ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na baadhi ya wanachama wakidai viongozi uongozi wa kitaifa muda wao ulikoma tangu mwaka jana.

Kwa mujibu wa Mrema, wajumbe 120 kutoka nchini nzima watahudhuria mkutano huo, atakaoufungua saa 6:00 mchana.

Kuhusu malamiko kwamba amekusanya mamluki wasio wajumbe kuhudhuria mkutano huo, ili kulinda maslahi yake, Mrema amesema “kuna watu wanafanya kampeni ya kueneza uongo dhidi yangu na chama change.”

“Wanaoeneza habri hizo chafu ni maadui zangu. Sasa hivi wana kampeni inayoitwa ‘Delete Mrema na TLP’. Lengo lao ni kuniharibia mimi na TLP,” amedai Mrema.

error: Content is protected !!