July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mramba, Yona kiporo

Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Mipango, Gray Mgonja (kushoto), Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona (katikati) na Waziri wa zamani wa Fedha Bazil Mramba

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo imeweka kiporo hukumu ya mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina, Gray Mgonja mpaka Julai 3 mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mawaziri hao wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 11.7.

Kuhairishwa kwa kesi hiyo kumetokana na kutokuwepo kwa Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja kati ya jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Jaji John Utamwa kwamba, hakimu huyo yupo Dodoma kikazi hivyo hukumu hiyo itasomwa tena atakaporejea.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Steward (ASSAYERS), Gorvanment Business Corporation kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.

Katika mashitaka hayo pia walidaiwa kuwa washtakiwa wakiwa watumishi wa serikali, Oktoba 10 mwaka 2003 walikaidi ushauri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa kuwataka wasitoe msamaha kwa kampuni hiyo.

Novemba mwaka 2008 washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Herzon Mwankenja na kusomewa mashtaka 13 likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka.

Hivyo, kesi hiyo ilipangiwa jopo hilo mahakimu na kuanza kusikilizwa mapema mwaka 2009.

Mashitaka hayo yalikuwa 13 ni pamoja na kutoa msamaha ovyo, kutumia vibaya madaraka, kuisababishia serikali hasara, kuruhusu kampuni kutolipa kodi, kutowajibika katika kazi zao.

Washtakiwa kwa wakati tofauti walikana mashitaka yote na kupelekwa rumande  katika Gereza la Keko  baada ya kushindwa kutimiza msharti ya dhamana.

Masharti hayo yalikuwa kujidhamini kwa kiasi cha Sh. Bil.3.9 kila mmoja, kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani na kuzuiliwa kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama hiyo.

Shariti la mwisho walitakiwa  kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na serikali kwa kila mmoja. Hata hivyo, baada ya kutimiza masharti hayo,  waliachiwa kwa dhamana hadi Ijumaa wiki hii hukumu itakaposomwa.

error: Content is protected !!