June 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mradi wa sungura kubeba wananchi

Spread the love

MRADI wa ufugaji sungara unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 23 Septemba mwaka huu, ili kuanza safari mpya ya ufugaji kwa wananchi jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya watu 1200 wanatarajia kunufaika, anaandika Pendo Omary.

Biubwa Maigo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency- inayoratibu mradi huo leo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, “mradi huo utafanyika jijini humo ambapo wanufaikaji watapata mitaji zaidi ya Sh 4.5 bilioni.

“Mradi huo utaleta mabadiliko makubwa, kwa sababu utawezesha wajasiliamali kuachana na dhana ya kuwa hawawezi kuwekeza ndani ya nchi yao,” amesema Maigo.

Maigo amesema, mradi huo utazinduliwa tarhere 23 mwezi huu na tayari kampuni hiyo imefanya utafiti wa kutosha na kujihakikishia upatikanaji wa wataalam na masoko ambapo wanufaikaji wataanza kulipa mkopo baada ya wanunuzi kununua sungura hao.

Aidha, Kampuni ya Mamaingo inajishughulisha na kuwatafutia wanachama wake ardhi iliyopimwa, kutoa elimu ya kilimo cha biashara, kusaidia upatikanaji wa masoko, mitaji ya kilimo na kuwasaidia Watanzania kuapata makazi bora.

 

error: Content is protected !!