Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mradi wa maji kumaliza tatizo la wananchi kuchangia maji na wanyama
Habari Mchanganyiko

Mradi wa maji kumaliza tatizo la wananchi kuchangia maji na wanyama

Spread the love

WAKATI zaidi ya 16, 000 wa vijiji vya Nyansenga, Kawekamo na Nyampande, Sengerema mkoani Mwanza wamesema wamekuwa wakiamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji mabondeni na kwenye visima, maji ambayo sio safi na salama kwa matumizi yao kutokana na kutumiwa na wanyama wakiwemo fisi na mbwa. Anaripoti Moses Mseti, Mwnaza … (endelea).

Wamesema kuendelea kutumia maji hayo ambayo linahatarisha usalama wa afya zao pamoja na wengine kuhatarisha uwezekano wa kuvunja ndoa zao pindi wanadamka kutafuta maji.

Hayo yamesemwa leo na mmoja wa wanawake wa kijiji cha Nyampande, Victoria Ibengwe wakati wa uwekaji saini wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata hiyo kati ya mkandarasi wa kampuni ya Halemu ya jijini Dar es Salaam na Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASSA).

Ibengwe alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakidamka usiku wa manane kuwahi kupanga foleni kwenye kisima cha asili lakini na kwamba kuja kwa mradi huo itakuwa ni mkombozi kwa vijiji hivyo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, akizungumza wakati wa tukio hilo muhimu kwa wananchi wa vijiji hivyo, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya maji kwa wakazi wa kata hiyo ya Nyampande.

Alisema kero ya maji katika vijiji hivyo ni ya muda mrefu licha ya jitihada za kuwafikisha huduma ya maji safi kuanza tangu mwaka 2013.

Mkurugenzi wa MWAUWASSA, Mhandisi Antony Sanga alisema mradi huo unaogharimu kiasi cha Sh. bilioni 1.8 utawanufaisha wakazi wapatao 16,000 katika vijiji hivyo vitatu wilayani sengerema.

Mhandisi  Sanga alisema tayari zabuni ya ununuzi wa mabomba ya utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande yamekwisha fanyika na kumpata mzabuni M/S Pipe Industries.

Alisema gharama za mabomba ya mradi huo ni zaidi ya Sh. 500 milioni huku kazi zitakazo tumika utandazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji kutoka kituo Cha cha mtambo wa kusukuma maji hadi kwenye tenki la kuhifadhia maji umbali wa kilomita sita.

Kazi nyingine zitakazo fanyika ni pamoja ujenzi wa kituo cha mtambo wa kusukuma maji Tabaluka chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha mita 30 kwa saa ( sawa na lita 30,00 kwa saa).

Pia utandazaji wa bomba za kasambaza maji aina ya HDPE zenye jumla ya urefu wa kilomita 43.0 na vipenyo kati ya milimita 50 hadi 160, ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo kuhifadhi  maji kiasi cha mita za ujazo 150 (sawa na lita).

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amemtaka mkandarasi wa kampuni ya HALEM kukamilisha mradi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika katika kujenga mradi wa maji kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo.

Mongella pia amewaomba wananchi kuwa na utaratibu wa kulipia huduma za maji ili mradi huo uwe endelevu pamoja na kumuagiza Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Sengerema kuunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kuendesha mradi kwa kuhusisha fani za mitambo na umeme.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!