June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mradi wa kuuvuruga Ukawa waiva

Prof. Ibrahim Lipumba (picha kubwa). Picha ndogo Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

Spread the love

MBUNGE wa Kaliua, Magdalena Sakaya, ametoa mwaliko kwa wabunge wote wa Chama Cha Mapinduzi, kuhudhuria tafrija na sherehe kubwa ya kuapishwa wabunge saba walioteuliwa na anayejiita, “mwenyekiti wa CUF,” Ibrahim Lipumba.

Mwandishi wetu kutoka Dodoma anasema, wa mujibu wa mwaliko huo, uliowasilishwa kwenye kikao cha wabunge wa CCM, kilichofanyika jioni ya leo.

Anasema, sherehe hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Didoma Hoteli.
Sakaya ambaye tayari amefukuzwa uanachama wa CUF, lakini akabaki kwenye chama hicho kwa maguvu ya serikali, amenukuliwa akimuahidi Spika wa Bunge, kuwa wabunge wake hao watafanya kazi bega kwa bega na uongozi wake.

Aidha, katika hatua nyingine, magari kadhaa yaliyobeba wafuasi wa Lipumba yameonekana maeneo ya Dodoma ili kuhudhuria kuapishwa kwa wabunge hao wasaliti.

Naye Lipumba ameonekana mjini hapa kuhudhuria sherehe hizo. Anatarajiwa kuingia bungeni kesho asubuhi.

error: Content is protected !!