Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mradi wa 630 milioni kufaidisha wakazi 12,500
Habari Mchanganyiko

Mradi wa 630 milioni kufaidisha wakazi 12,500

Spread the love

 

ZAIDI ya wakazi 12,500 wa vijiji vya Milola na Mavimba Wilayani Ulanga mkoani Morogoro wanatarajia kunuafaika na mradi wa maji wenye thamani ya Sh. 630 millioni unaotekelezwa na Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira vijiji (RUWASA). Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizingumza katika mradi huo Meneja wa Ruwasa Wilayani ya Ulanga mkoani hapa Mhandisi Mbaraka Kilangai wakati mradi huo ulipotembelewa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru alisema mradi huo utakaogharimu kiasi cha Sh. 630 milioni unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu ambao hadi sasa umefikia asilimia 95 ya kukamilika.

Mhandisi Kilangai alisema mradi wa maji Milola -Mavimba pia umewasaidia wananchi hao kuwaepusha na kupata magonjwa ya milipuko yatokanayo na matumizi ya maji yasiyokuwa salama.

Naye Mbunge wa Ulanga, Salim Hasham ameishukuru Serikali kwa kutoka fedha kwa ajili ya utekelezaji uboreshaji na ufufuzi wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.

Hasham alisema utekelezaji wa miradi ya maji katika jimbo hilo utasaidia wananchi kupata maji safi na salama tofauti na awali ambapo walitumia maji ya mito visima na wakati mwingine mabwawa na hivyo kuwa hatarini kupata magonjwa mbalimbali.

Awali kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdallah Shaib amewataka wakazi wa maeneo ya jirani na mradi huo kuhakikisha wanatunza na kuhifadhi mazingira ili chanzo hicho kiwe endelevu kwa manufaa ya wote.

Shahib alisema miradi yoyote ile inapaswa kutunzwa na kulindwa sababu kinyume chake ni uharibifu ambao unaipa hasara kubwa Serikali ambayo imetumia fedha nyingi kukamilisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!