May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mradi umeme Biharamulo kukamilika Machi 2021- Serikali

Mafundi umeme wakiwa kazini

Spread the love

 

MRADI wa kujenga kituo kidogo cha umeme cha Nyakanazi (KV 220), kutoka Rusumo na Geita unatarajiwa kukamilika Machi mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ni kauli ya serikali baada ya Injinia Ezara Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo Magharibi kuhoji, lini mradi huo ungekamilika.

Mbunge huyo awali aliieleza wizara hiyo kwamba, kumekuwepo na idadi kubwa ya watu wanaotumia umeme kwenye Wilaya ya Biharamuloihi vyo kusababisha tatizo la umeme kukatika mara kwa mara kwa umeme huo.

Kutokana na tatizo hilo, aliiohji serikali kwamba ni lini mradi huo utakamilika ili kuondoa tatizo hilo la kukatika katika kwa umeme?

Wizara ya Nishati na Madini imemueleza, serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), inatekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovolti 220 kutoka Geita hadi Nyakanazi.

“Mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Geita – Nyakanazi, yenye urefu wa kilometa 144 ambapo Mkandarasi Kampuni ya M/S Kalpataru Power Transmission Ltd kutoka nchini India, anaendelea na kazi za mradi,” imeeleza wizara hiyo.

Na kwamba, hadi sasa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupoza umeme, umefikia asilimia 60.

“Gharama ya mradi ni EURO milioni 45 sawa na takriban shilingi bilioni 117.79. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi Machi 2021.

“Ni mategemeo ya serikali kuwa mradi utakapokamilika utaimarisha na kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika maeneo ya Wilaya ya Biharamuro,” imeeleza wizara hiyo.

error: Content is protected !!