August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpole aibuka mfungaji Bora Ligi Kuu

George Mpole

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Geita Gold, George Mpole ameibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa na mabao 17, huku akimuacha Fiston Mayele mwenye mabao 16. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ilimlazimu Mpole kusubiri mpaka mchezo wa mwisho wa Ligi, kufuatia kuwa katika kinyang’anyiro kikali na Mayele kwenye Ligi Kuu hasa kwenye mzunguko wa pili.

Huu ni msimu wa pili kwenye Ligi Kuu kwa mzawa kuchukua kiatu cha ufungaji bora, kufuatia msimu uliomalizika, John Bocco, nahodha wa klabu ya Simba alifanikiwa kutwaa tuzo hiyo akiwa na mabao 16.

Kiwango kilichooneshwa na mshambuliaji huyo, huenda msimu ujao akaonekana katika moja ya timu kubwa zinazoshiriki Ligi Kuu, kutokana na ubora aliokuwa nao.

Mpole huu ni msimu wake wa pili akitumikia klabu ya Geita Gold, ambayo alipanda nayo daraja kutoka Ligi daraja la kwanza msimu uliomalizika.

error: Content is protected !!