Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mpogoro ahamasisha sensa
Habari Mchanganyiko

Mpogoro ahamasisha sensa

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogoro amewahamasisha vijana katika wilaya hiyo kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Same… (endelea).

Mpogoro amefanya hamasa hiyo alipokua akizungumza na vijana zaidi ya 1,800 waliokua kwenye kambi ya Kanisa la Waadventisti Wasabato Kanda ya Kaskazini iliyofanyika Alkachenje wilayani hapo.

o katika kambi hiyo walishiriki kwenye zoezi la uchangiaji damu kwa hiari na kupata chanjo ya Uviko-19.

 

Mpogoro amewataka kuendelea kutoa elimu kwa vijana wenzao walio mitaani umuhimu wa kupata chanjo na kutoa damu ili kuweza kusaidia wananchi wengine.

“Lengo la kuzungumza na nyinyi kuelimisha vijana kuanzia miaka 10-35 umuhimu wa sensa ya mwaka huu na kutoa elimu ya Uviko-19 kwa vijana walioshiriki mafunzo hayo ambao wamechangia damu kwa hiari na kuchanja chanjo ya Uviko-19 kwa wale wenye umri wa kuanzia miaka 18,” alisema.

Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Same, Dk. Alex Alexander amewashukuru vijana wote wenye umri kuanzia 18-35 walioshiriki kikamarifu zoezi la kuchangia damu kwa hiari na kupata chanjo ya Uviko-19 kuwataka vijana hao kutoa elimu kwa vijana wenzao majumbani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miito na Malezi wa Kanisa la Advetist Wasabato Conference ya Kaskazini Mchungaji Mao alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea Kambini na kutoa Elimu.

Mchungaji Mao alimpongeza na kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba amekuwa kiungo muhimu cha kujenga umoja na mshikamano Tanzania na wao kama viongozi wa dini watamuombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!