SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), leo 9 Novemba 2020, linatarajia kupanga droo ya michezo ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika huku mwakilishi pekee kwenye michuano kutoka nchini Tanzania ni klabu za Simba mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2019/20. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Droo hiyo itapangwa hii leo kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliopo Cairo, nchini Misri majira ya kwa msimu mpya wa mashindano 2020/21.
Klabu ya Simba itaanza mbio hizo kwenye hatua ya awali kwa kucheza michezo miwili na wakifanikiwa kuvuka hapo itaingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo kama walivyofanya kwenye msimu wa 2018/19.
Sambamba na droo hiyo, pia Caf watatangaza tarehe ya kuchezwa kwa mechi hizo ambapo zitakuwa kwenye mtindo wa nyumbani na ugenini licha baadhi ya timu kutoanzia kwenye hatua hiyo.
Timu ambazo hazitoshiriki kwenye hatua hiyo ya awali ni Al Ahly na Zamalek za Misri, AS Vital Club na TP Mazembe zote kutoka Congo, Waydad AC na Raja Casablanca za nchini Morocco, Esperance (Tunisia), Mamelod Sundowns (Afrika kusini), Horoya na Primerio De Agosto kutoka Angola.

Aidha Shirikisho hilo pia litapanga Droo ya michezo ya kombe la Shirikisho ambapo klabu ya Namungo Fc kutoka Luangwa, Lindi ndio timu pekee itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa ndani ya bara la Afrika.
Mara ya mwisho Simba kushiriki michuano ya klabu bingwa ilikuwa msimu wa 2019/20 na ikatolewa kwenye michezo ya awali dhidi ya UD Songo ya kutoka Msumbiji.
Leave a comment