July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpina wanaponda watia nia wenzake

Spread the love

MBUNGE wa Kisesa, Luhanga Mpina (CCM), amewaponda baadhi ya watangaza nia wenzake ambao hawakuhudhuria wakati wa uwasilishwaji wa Bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2015/16. Anaandika Dany Tibason, Dodoma…(endelea).

Amesema ni dalili za wagombea hao kutokuwa na maandalizi ya kutosha na kwamba hawajiamini.

Mpina ametoa kauli hiyo leo, wakati akifungua semina ya wabunge iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu Tanzania kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania kwa kipindi cha miezi minne iliyopita.

Mpina ambaye amechukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama chake cha CCM ili aweze kupeperusha bendera ya kuhusaka urais, amesema Rais makini ambaye anataka nchi iwe na uchumi imara hawezi kuikimbia bajeti ambayo inatakiwa kutumiwa kwa mwaka mmoja kabla ya kutengeneza bajeti mpya.

Mbunge huyo aliye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, amesema amelazimika kuwepo bungeni kwa kipindi chote ili kuhakikisha anaifuatilia bajeti hiyo ili iweze kutatua matatizo ya Watanzania.

“Waheshimiwa wabunge mnajua wazi ya kwamba mimi nimetangaza nia ya kuwania nafasi ya urais lakini nipo hapa kwa lengo la kuhakikisha nafuatilia bajeti hii nione kama inaweza kuwa baraka kwa Watanzania.

“Rais makini ambaye anajua wazi kuwa wananchi wake wanatakiwa kuishi vizuri, hawezi kuondoka na kuiacha bajeti bila kuifuatilia ili kujua nini kinachofanyika.

“Sasa ukiona mtu anakimbia na kuiacha bajeti hii muhimu kwa Watanzania, unatakiwa kutia shaka juu ya maandalizi ya mtu huyo, hata mimi nadhani wale wote waliotangaza nia ya kugombea urais hawana maandalizi ya kutosha na hawajiamnini na ndiyo maana wanakimbia kimbia ovyo,”alisema Mpina.

Wakati akizungumza na wabunge hao, huku waliowengi walionekana kumpigia makofi ya kishabiki, ilithibitika mawaziri waliotangaza nia, wengi hawakuhudhuria.

error: Content is protected !!