April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mpina avunja bodi ya maziwa

Spread the love

UTENDAJI mbovu wa Bodi ya Maziwa, umemsukuma Luhaga Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania kuvunja bodi hiyo. Anaripoti Hamisi Mguta…(endelea).

Katika taarifa yake leo tarehe 22 Agosti 2019 Mpina amesema, amechukua uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa bodi hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza, Waziri Mpina amepewa mamlaka ya kuchukua uamuzi huo chini ya Sheria ya Bodi ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2014 kifungu cha 8 na 9 (1).

Miongoni mwa majukumu ya bodi hiyo ni pamoja na kuhamasisha, kusimamia na kuendeleza uzalishaji, usindikaji na uuzaji wa maziwa.

error: Content is protected !!