January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpina atia mguu urais, aahidi kuongeza mapato

Mbunge Luhaga Mpina, akiwa katika mkutano wa hadhara

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, akitangaza nia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mwandoya.

Spread the love

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, atangaza nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuomba uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili agombea urais wa nchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, huku akitamba kwamba anataka kusimamia mapato ya Serikali. Anaandika Moses Mseti, Simiyu … (endelea).

Mpina ambaye ameingia katika mbio hizo kwa kushtukiza, anaongeza orodha ya makada wa CCM waliotangaza rasmi. Hadi sasa waliojitangaza ni Edward Lowassa, Mwigullu Nchemba, Stephen Wassira, Lazaro Nyalandu, Dk. Khamis Kigwangallah na leo wataongezeka Prof. Mark Mwandosya na Makongoro Nyerere.

Mpina ametangaza uamuzi huo jana jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwandoya jimboni Kisesa, akisema kutokana na kujipima na kutafakari, ameona anayo nafasi na uwezo wa kuingia katika kinyang’ang’aro hicho.

Amesema wengi waliotangaza nia ya kugombea urais, hawana uwezo na wameshindwa kuainisha mambo mhimu yatakayoingizia taifa kipato na kukuza uchumi.

Kwa mujibu wa Mpina, kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha anasimamia ukusanyaji wa kodi ambao umeshindwa kufanywa na marais waliopita, pia kusimamia ulipaji wa kodi bandarini.

“Watangaza nia wote waliotangaza sijaona hata mmoja ambaye amezumgumzia kusimamia ukusanyaji wa kodi, kwani huwezi kujenga barabara na vituo vya afya bila kukusanya kodi.

“Ukusanyaji wa mapato serikalini upo chini sana na hiyo yote ni kwa sababu ya usimamizi mbovu iliopo kwa watumishi wa umma, lakini nitahakikisha tunakusanya mara tatu ya hapa,” amesema Mpina.

Ameongeza kuwa, atahakikisha anasimamia ubadhilifu wa fedha za umma serikalini, watumishi kuidhinisha fedha za umma katika matumizi hewa pamoja na utoroshaji wa fedha kwenda nje ya nchi.

Hata hivyo, amesema kuwa serikali imeshindwa kufuatilia na kuwakamata watu waliikopa zaidi ya Sh. 2 billioni, ambazo zimekopwa na kusababisha watanzania kukosa maendeleo kwa muda mrefu.

Mpina amesema kuwa, kushindwa kuwepo kwa usimamizi mzuri wa rasilimali hizo kumesababisha kuwepo kwa wimbi la vijana mtaani wasiokuwa na ajira.

“Kama nikipewa nafasi ya kuwa Rais, nitahakikisha vijana wote wanapata ajira na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kupunguza utegemezi uliopo hivi sasa,” alisema Mpina.

Pia amegusia suala la afya nchini, akisema viongozi wanaoshindwa kuwapeleka watoto wao katika hospitali za serikali ndio wamekuwa wakisababisha kurudusha nyuma sekta ya afya.

Amedai kuwa watumishi wengi hususani wabunge, waopeleka watoto wao kutubiwa nje ya nchi wanasababisha watoto wa maskini kuishi katika mazingira hatarishi ya afya zao.

“Kwenye serikali yangu sitakubali kuona mambo ya aina hiyo yanaendelea kuwepo na nitasimamia watumishi wote wanaotumia vibaya fedha za umma wanachukuliwa hatua na wale wote wanaodaiwa kuiba wakusanye virago vyao mapema,” ameainisha Mpina.

error: Content is protected !!