Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina atamba kuvuka malengo ya makusanyo
Habari za SiasaTangulizi

Mpina atamba kuvuka malengo ya makusanyo

Spread the love

WAZIRI wa Mifigo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake itahakikisha inavuka lengo la makusanyo kwa kukusanya kiasi cha Sh. 50 bilioni badala ya Sh. 20 bilioni ambazo ndilo lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2018/19. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Mpina alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha tathimini juu ya upotevu wa mapato kupitia kwa sekta ya mifugo, kikao hicho kilifanyika jijini hapa.

Mpina amesema kuwa mapato mengi yatokanayo na mifugo yanapotea kutokana na kutokuwepo kwa uthibiti wa utoroshaji wa mifugo ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uthibiti wa kutosha katika utozaji faini na kodi zilizo halali.

Mpina amesema kuwa sekta ya mifugo imekuwa ikipoteza mapato mengi na kusababisha wizara kutokuwa na fedha za kutosha licha ya kuwa Tanzania ni nchi ya pili afrika kwa kuwa na mifugo mingi na kujikuta wizara inashindwa kupata hata hela za kulipa mishahara.

Amesema kuwa kwa miaka mingi sekta ya mifugo imekuwa ikikusanya kiasi cha Sh. 10 hadi 12 bilioni na kulisababishia taifa kuwa na faida yoyote inayotokana na sekta ya mifugo, jambo ambalo lilikuwa linatokana na kutokuwa na makusanyo yenye uthibiti sahihi.

Waziri huyo amesema kuwa mifugo mingi ya Tanzania imekuwa ikinufaisha nchi za jirani kutokana na baadhi ya watanzania kutorisha mifugo na kuingiza katika nchi za jirani ambako huko mifugo hiyo hutozwa ushuru halali pamoja na kodi zote ambazo zinastahili kutozwa tofauti na Tanzania ambapo mifugo mingi haitozwi ushuru halali pamoja na kutotozwa kodi inayotakiwa.

Aidha Mpina amesema kuwa kwa muda wa miezi mitatu kwa mwaka wa fedha ulioisha Wizara imeweza kukusanya kiasi cha Sh. 7.1 bilioni na kueleza kuwa kwa miezi tisa Wizara imeweza kupoteza kiasi cha Sh. 21.5 bilioni na kwa mwaka zimepotea Sh. 28.7 bilioni.

Aidha Mpina, ameagiza kuandaliwa kwa mkakati wa udhibiti wa mapato yanayotokana na sekta hiyo kwa lengo la kukusanya kiasi cha Sh. 20 bilioni au zaidi.

Ambapo ndani ya miezi mitatu imekusanya bilioni saba katika operesheni Nzagamba iliyoanza kufanyika mwezi aprili mwaka huu iliohusisha maafisa mifugo kutoka katika kanda zote Nchini.

Mpina alimuagiza mkurugenzi wa huduma za mifugo kuanza mpango mpya wa kudhibiti uingizaji wa madawa ya mifugo Nchini na katika zoezi la uagizaji dawa na usambazaji maofisa maduhuri uvuvi na mifugo ni lazima waingie maeneo husika.

Amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi sio Wizari ndogo na ina umuhimu zaidi hivyo wizara hiyo ilipewa rungu na kamati kufanya opereshe nzagamba kutokana na operesheni hiyo kuongeza kipato cha Taifa.

Katika hatua nyingine aliagiza ofisi ya mkurugenzi kuanzishwa kwa kitengo cha kuthibiti utoroshwaji wa rasilimali zitokanazo na mazao ya mifugo, huku Mpina akitangaza kuwa Pareishen Nzagamba itaendelea ifikapo Agost mwaka huu.

Katika mjadala huo maafisa operesheni Nzagamba waliorozesha changamoto wanazokumbana nazo katika operesheni hiyo ikiwa ni wafanyabiashara kukatiwa ushuru kwa njia za mkato na wasafirishaji kutokuwa na leseni pamoja na vibali vilivyokwisha muda wake.

Pia watumishi kukosa vitendea kazi na kuwa watumishi wachache katika operesheni hivyo kusababisha mapato mengi kupotea.

Mapendekezo makuu yalikuwa kuunda vikosi vya kudhiti kushirikiana na idara ya uhamiaji kuongeza udhibiti wa utoroshaji wa mifugo nje ya nchi kupitia njia za panya na kukamilisha ujenzi wa minada ili kupata makusanyo ya ushuru mazuri.

Waliiomba serikali kutoa fedha kwaajili ya uendeshaji zoezi la utoaji wa elimu kwa wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo katika operesheni hiyo kwani wengi wao hawana elimu juu ya uendeshaji wa bihashara hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mohamud Mgimwa amesema kuwa Oparesheni Nzagamba 201 inayofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni sahihi na ina tija na iwe endelevu.

Amesema kuwa kamati na bunge kwa ujumla wamebariki kinachofanywa na wizara hiyo kwani wizara imekuwa ikipoteza mapato mengi kutokana na kutokuwepo kwa oparesheni za mara kwa mara jambo ambalo kimsingi serikali inapoteza mapato mengi.

Aidha amesema kwa sasa kinachotakiwa ni kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wafugaji na jamii kwa ujumla wake.

Naye mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Kunti Majara amesema kuwa licha ya Operesheni Nzagamba kuwa ni nzuri na yenye manufaa lakini bado imekuwa ikifanyika bila kutoa elimu kwa jamii na wafugaji kwa ujumla wake.

“Kuna tatizo kubwa ambalo linafanyika hizi opareisheni zimekuwa zikifanyika bila kuwashirikisha wananchi, jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa na kuichukia serikali yao.

“Kama elimu na ushirikishwaji vingekuwa vinafanyika kabla ya kuanza kwa Opareisheni hiyo pasingekuwepo na tatizo lolote au malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wafugaji wa kulalamikia zoezi zima la ufugaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!