Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina ataka uchunguzi mchakato wa manunuzi SGR Tabora-Kigoma
Habari za Siasa

Mpina ataka uchunguzi mchakato wa manunuzi SGR Tabora-Kigoma

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
Spread the love

 

MBUNGE wa Kisesa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luhaga Mpina, ameliomba Bunge kuitisha mchakato wote wa manunuzi wa mkataba wa mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Tabora-Kigoma kutokana na ongezeko kubwa la gharama za mradi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Mpina amesema mkataba wa ujenzi wa kipande hicho baina ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) umetolewa kwa mfumo wa chanzo kimoja (Single source) badala ya ushindani.

Mbunge huyo ambaye amekuwa machachari katika kuibana serikali kwenye utekelezaji wa shughuli zake, amesema kwa ukubwa wa mradi huo wa Sh 6.34 trilioni haukupaswa kutolewa kwa mfumo wa chanzo kimoja.

Aidha amesema kampuni hiyo imepewa kazi hiyo wakati ambao ina kazi nyingine ya ujenzi wa kipande cha Mwanza-Isaka, ambapo amedai “haijajenga hata kilometa moja.”

Vilevile amesema mkataba huo unatia mashaka kutokana na utofauti mkubwa wa gharama za ujenzi ikilinganisha na ile ya kipande cha Mwanza-Isaka kilomita 341 inayojengwa kwa Sh. 3.12 trilioni.

“Kumekuwa na utofauti mkubwa wa gharama za mradi wa Tabora-Kigoma ambao unajengwa kwa Trilioni 6.43 wastani wa kilomita 1 kwa Sh 12.5 bilioni wakati kampuni hii hii inajenga Mwanza-Isaka kilomita moja kwa Sh 9.1, tofauti ya Sh 3.4 bilioni kwa kilomita,” amesema Mpina na kuongeza;

“Naomba bunge liazimie mambo yafuatayo kwanza tuitishe mchakato wote wa manunuzi kuanzia mwanzo wa kutangazwa hadi utoaji…pili ufanyike ukaguzi maalumu wa CAG, PPRA na PCCB kukagua na kutoa taarifa ya ukaguzi juu ya kile kilichofanyika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!