Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Mpina ashauri mabadiliko utaratibu wa kupitisha bajeti, Spika ampa darasa
Habari

Mpina ashauri mabadiliko utaratibu wa kupitisha bajeti, Spika ampa darasa

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Kisesa nchini Tanzania amelishauri Bunge kubadilisha utaratibu wa kupitisha Bajeti ya Serikali kwa kukamilisha kwanza Sheria ya Fedha kisha kupigia bajeti kura. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mpina amesema utaratibu wa sasa unakinzana kwani mbunge anaweza kupiga kura kwenye bajeti na kisha kuja kukosoa kwenye Sheria ya Fedha ambayo itaathiri bajeti iliyopitishwa tayari.

Akichangia Mswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022 leo Jumanne tarehe 28 Juni, 2022, Mpina amemshauri Spika Dk. Tulia Akson kuhakikisha mabadiliko hayo yanafanyika ili kuongeza ufanisi zaidi katika upitishaji wa bajeti.

Hata hivyo Spika Tulia alitoa ufafanuzi kuhusiana na hoja ya Mpia na kusema ngazi iliyofikiwa ya kutunga Sheria ni kufanya marekebisho ya vifungu na si kutoa wazo jipya.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Alisema Muswada huo ulishawasilishwa kwa wabunge na ulipaswa kurekebishwa sambamba na mambo mengine.

“Ngazi hii inabidi uje na kifungu wewe unasemaje na uwe umeleta marekebisho kwasababu tumeshafika mwisho kama hujaleta marekebisho halafu una mawazo yako, hata Waziri hapa mbele haji kuyajibu…yeye atajibu vifungu ambavyo tumeleta mabadiliko.

“Kwahiyo ngazi hii tupo kwenye kutunga Sheria na tunaangalia vifungu yale tunayotaka yarekebishwe, tulishapewa hii (Muswada) mapema unakuwa umeshaleta na hapa ninayo ya Serikali ambayo wamekubaliana na Kamati na ninayo ya mbunge mmoja tu ambaye yeye hajakubaliana na kifungu kaleta marekebisho yake,” alifafanua Dk. Tulia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!