Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Mpina apinga uanzishwaji mahabusu za watuhumiwa dawa za kulevya
Tangulizi

Mpina apinga uanzishwaji mahabusu za watuhumiwa dawa za kulevya

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
Spread the love

 

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amepinga uanzishwaji wa mahabusu za watuhumiwa wa dawa za kulevya pamoja na masharti ya kumuweka mtu kizuizini kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa katika sheria nyingine kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akichangia Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, sura ya 95 leo tarehe 14 Septemba, 2022 jijini Dodoma, Mpina amesema mahabusu hizo zinaweza kutumika kuwatesa na kuwalazimisha watuhumiwa kukubali makosa.

Marekebisho hayo yamewasilishwa bungeni leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Eliezer Feleshi ambapo pamoja na mambo mengine katika ibara ya 13 ya muswada huo umekifuta kifungu cha 32 na kukiandika upya kama kifungu cha 32 (4)(5) kinachotoa masharti kwa Mamlaka ya Kuzui na Kudhibiti Dawa za Kulevya uwezo wa kuanzisha mahabusu hizo.

Pia sheria hiyo imetoa uwezo kwa mamlaka hiyo kukamata, kupekua na kuchunguza makosa yaliyo chini ya Sheria hiyo.

Hata hivyo, Mpina amesema licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kidhibiti dawa za kulevya nchini, jambo hilo la uanzishwaji wa mahabusu za watuhumiwa wa dawa za kulevya linapaswa kufanyika kwa umakini.

“Unapotaka kuanzisha mahabusu zako kwa ajili ya nini? ulazima wa kuanzisha mahabusu zako kwa ajili ya nini?. Ina maana mahabusu zilizopo polisi na magereza hazina uwezo wa kudhibiti watuhumiwa na kama hazina basi zinapaswa kuboreshwa.

“Leo tunataka kuwakabidhi mamlaka watunze mahabusu, hawa mahabusu wana utaratibu wake wa namna ya kutunzwa, sasa kama kila mtu anataka kutunza mahabusu wake itakuaje.

“Kama msimamizi akipewa mpaka mamlaka ya kukaa na watuhumiwa, wapo watu watalazimishwa kukiri, ushahidi tunao… zipo mamlaka tulizipa mamlaka kutunza ushahidi mahakama, mfano TAWA wakakaa na mifugo ya wafugaji, ikafa mikono mwao,” amesema.

Amesema Bunge likitunga sheria za aina hiyo taasisi nyingine za Serikali kama Takukuru, Uhamiaji na nyingine zinazoshughulika na majangili nazo zitatakuanzisha mahabusu kisha nchi kutapaa mahabusu kila mahali.

Pia amehoji fedha za ujenzi wa mahabusu hizo kwamba zitatoka wapi ilihali hadi sasa kuna wilaya nchini hazina mahabusu za polisi wa magereza.

Aidha, badala yake amependekeza kufanyike ukarabati wa mahabusu za polisi na magereza zilizopo ili ziwe na vigezo vya kupokea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

George Simbachawene

Hata alipopewa taarifa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene kwamba mahabusu za watuhumiwa wa dawa za kulevya ni tofauti na mahabusu wale wa makosa mengine, Mpina alikataa hoja hiyo.

“Binadamu wana maarifa makubwa, anaweza kumeza kete zikakaa tumboni, hivyo akatakiwa kukaa kwa muda fulani, ndio maana chombo hiki (mahabusu) kinakuja na mazingira mahususi kwa watuhumiwa wa aina hii,” amesema Simbachawene.

Hata hivyo, baada ya kumaliza mchango wake, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alimhoji Mpina kama amewasilisha mapendekezo mbadala na kujibu kwamba atayawasilisha.

Spika amemueleza kuwa mchango wake hautapinga mapendekeo hayo ya Serikali kwa kuwa hajawasilisha mapendekezo mbadala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!