Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Mpango wa tatu wa maendeleo wazinduliwa, kutumia Trilioni 114.8
Tangulizi

Mpango wa tatu wa maendeleo wazinduliwa, kutumia Trilioni 114.8

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amezindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26, utakaogharimu Sh. 114.8 trilioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021 jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, ikiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Majaliwa amesema mpango huo umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya miaka 25 (2000 hadi 2025), Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/25, matokeo ya tafiti zilizofanywa na vyuo vikuu pamoja na taasisi za elimu.

“Tunapoelekea kuzindua mpango huu wa tatu, umezingatia dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025, imezingatia ilani ya CCM, mpango elekezi wa muda mrefu wa 2011/12 hadi 2025/26, sera na mikakati ya kisekta, matokeo ya tafiti zilizofanywa na vyuo na taasisi, dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ) ya 2050,” amesema Majaliwa.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni, amesema utekelezaji mpango huo utashirikisha makundi ya wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali.

“Mpango huu ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha maendeleo ya nchi yetu kupitia ahadi za ilani ya CCM, yanapatikana.”

“Mpango huu unashirikisha kikamilifu makundi ya wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mpango huu ni jumuishi na umezingatia mahitaji ya watu,” amesema Mhandisi Masauni.

Akielezea utekelezwaiji wa mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, amesema takribani Sh.114.8 trilioni zitatumika, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kutoa Sh.40.6 trilioni huku Serikali ikitoa Shj. 74.2 trilioni.

“Vipaumbele vya mpango vinatarajiwa kugharimu Sh.114.8 trilioni, sekta binafsi itatoa Sh. 40.6 trilioni na sekta ya umma Sh. 74.2 trilioni. Mchango wa sekta binafsi unatarajiwa kutokana na miradi ya pamoja kati ya sekta nbinafsi na umma,” amesema Tutuba.

Katibu Mkuu huyo wa Hazina amesema, fedha hizo zitatokana na mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, misaada na mikopo kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema mpango huo una maeneo makuu ya matano ya kipaumbele, ambapo eneo la kwanza ni ukuzaji uchumi shindanishi na shirikishi.

“Mpango wa tatu umejikita katika maeneo makuu matano ya kipaumbele, la kwanza imejielekeza kwenye kuchochea uchumi shindani na shirikishi.”

“Katika eneo hili, Serikali itahakikisha uwepo wa utulivu wa viashria wa uchumi jumla na ujenzi wa uchumi jumuishi, wenye uwezo na ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa,” amesema Tutuba.

Tutuba ametaja eneo la pili ni “eneo la pili umejielekza kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa viwanda na utoaji huduma. Umejikita kujumuisha miradi inayolenga kuongeza thamani na kuzalisha bidhaa zinazotumia malighafi za ndani kutoka sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, mifugo na madini.”

Tutuba amesema eneo la tatu ni ukuzaji uwekezaji na biashara, ambapo Serikali inalenga kuimarisha program za kuimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Eneo la nne ni kuchochea maendeleo ya watu kwa kutekeleza miradi inayoboresha maisha ya wananchi, huku la mwisho na kuendeleza rasilimali watu kwa kuweka mikakati inayolenga kuendeleza ujuzi na rasilimali watu.

Tutuba amesema, mpango huo uemanisha mfumo wa ufuatiliaji na tathimini kwa ajili ya kuwezesha wajibikaji, kulinda thamani ya fedha inayotumika na kutoa mafunzo wakati wa utekelezwaji wake.

Mpango huo wa tatu wa maendeleo, unatarajiwa kuanza kutumika Julai Mosi mwaka huu hadi Juni 2026, baada ya mpango wa pili wa maendeleo kufika tamati kesho tarehe 31 Juni 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!