July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpango wa Rais Kikwete kujenga reli Dar wapingwa

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Spread the love

MPANGO Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuitaka serikali ya Jamhuri ya India, kutoa msaada wa kujenga Reli jijini Dar es salaam ili kupunguza foleni, umepinga na baadhi ya wananchi na kuita, “usanii wa karne.”

“Ni Kikwete huyuhuyu ambaye miaka 10 iliyopita, aliahidi kujenga reli ya kisiasa ya kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda. Ni huyu aliyeahidi ujenzi wa reli kwenda Kenya; na au Kigoma na Mwanza. Lakini mpaka sasa, hakuna kilichofanyika.

“Sasa ikiwa leo, miezi mitatu kabla ya kuondoka Ikulu, ndiyo  anakuja na hadithi hii ya reli ya Dar es Salaam? Huu ni usanii wa kupitiliza,” ameeleza Juma Amiri, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waziri Mkuu wa India, Pranad Mukherjee jana mjini New Delhi, Rais Kikwete alisema, anaomba nchi hiyo isaidie ujenzi wa reli hiyo ili kuondoa msongamano wa magari katikati ya jiji.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanakebehi kauli hiyo ya Kikwete kwa madai kuwa, imelenga kuwaghiribu wananchi.

error: Content is protected !!