
Daraja la Mpui Mpanda
SHILINGI 4.5 bilioni zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara Mpanda–Uvinza kwa kiwango cha lami. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, alipokuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema).
Afri alitaka kujua ni lini serikali itaweza kujenga na kukamilisha barabara kutoka Mpanda hadi Uvinza kwa kiwango cha lami kwa lengo la kuunganisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Katika majibu yake, Mhandisi Lwenge, amesema kuwa barabara ya Mpanda-Uvinza yenye urefu wa kilometa 194 ni sehemu ya barabara kuu ya Tunduma-Sumbawanga-Mpanda–Uvinza-Kasulu–Nyakanazi.
Ameongeza kuwa, serikali imetenga Sh. 4.5 bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Mpanda-Uvinza ambapo awamu ya kwanza itahusisha sehemu ya barabara kutoka Mpanda–Usimbili yenye urefu wa kilometa 30.
“Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo ametangazwa na uchambuzi wa zabuni unaendelea kwa ajili ya kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami,”amesema.
More Stories
Barrick ilivyoshiriki katika kuadhimisha Siku ya Canada
PURA yaanzisha kanzidata
Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania