January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpambe wa Lowassa aenguliwa UDOM

Spread the love

BALOZI Dk. Agustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokana na aliyekuwa ameshika nafasi hiyo Balozi Juma Mwapachu kumaliza muda wake. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alitoa kauli hiyo leo alipozungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mahafari ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 na 27 mwaka huu.

Amesema kuwa Balozi Mwapachu amemaliza muda wake tangu Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Balozi Mahiga ni mzoefu katika utumishi na amefanya kazi nzuri nje na ndani ya nchi huku akiwa na matumaini makubwa kwamba ataliongoza baraza hilo bila hofu yeyote.

Hata hivyo amesema Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amemuongezea muda wa miezi sita, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Shaban Mlacha ambaye alipaswa amalize muda wake Desemba 30, mwaka huu.

Amesema, uamuzi wa kumuongezea muda Profesa Mlacha, umetokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi ambayo ilianza chini ya uongozi wake ukiwemo mradi wa umeme jua ambayo ameona abaki ili angalau aifikishe mahali pazuri.

“Profesa Mlacha na Naibu Makamu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Ludovick Kinabo waliongezewa muda walioongezewa unaisha Desemba 30 mwaka huu, lakini Mlacha ataendelea kuwepo kwani ameongezewa miezi sita mingine ili asogeze miradi aliyoianzisha,” amesema Profesa Kikula.

Kuhusu mahafali amesema, jumla ya wahitimu 4,136 wa kada na ngazi mbalimbali watatunukiwa vyeti idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na wahitimu 3,949.

Amesema, tangu kuanzishwa kwa chuo, idadi ya wahitimu kuanzia mahafali ya kwanza mwaka 2010 ni 26,663 huku akisema idadi hiyo ni kubwa hali inayohitaji ubunifu ili vijana wanaosoma katika chuo hicho waweze kuajiriwa na kujiajiri.

error: Content is protected !!