September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpalestina azindua gari la umeme

Spread the love

JIHAD Mohammed, Mpalestina na mmiliki wa Kampuni ya Electra iliyopo Lebanon, amezindua gari linalotumia umeme. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea)

Uzinduzi huo, unafanyika kwa mara ya kwanza katika Historia ya Palestina, ambapo mfanyabiashara huo amesema, uzinduzi huo ni rafiki wa mzingira.

Mradi huo wa kihistoria, umefanywa kwa ushirikiano wa wahandisi wa Palestina na Lebanon.

Kampuni ya Electra imelipa gari la “QUDS” ambalo ni jina la kiarabu lenye maana ya Jerusalem.

Kampuni ya Electra imisema “kwamba hili ni gari la kujivunia ambalo litaingia katika masoko ya kimataifa katika miaka michache ijayo.

“Gari hili lina ubora wa hali ya juu kwa sababu limeundwa na kaboni ya kilele cha kaboni ambayo hutumiwa na shirika la NASA (Shirika la Anga la Marekani).”

Mohammed amesema, kampuni yake imeipa gari hilo jina la ‘QUDS’ ikimaanisha Yerusalemu ili kuongeza ufahamu wa swala la Palestina ulimwenguni.

error: Content is protected !!