Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Mourinho, Lampard,Solskjaer vitani tuzo ya kocha bora
Michezo

Mourinho, Lampard,Solskjaer vitani tuzo ya kocha bora

Spread the love

MAKOCHA vigogo katika Ligi Kuu England, Jose Mourinho, Frank Lampard na Ole Gunna Solskjaer ni miongoni mwa makocha wanne walio kwenye kinyang’anyiro cha kugombea tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Makocha hao wameingia kwenye orodha hiyo baada ya kuongoza timu zao kwenye michezo 14 ya ligi hiyo, huku David Moyes akiingia baada ya kuingoza Everton katika michezo 11 ya Ligi Kuu na kufanikiwa kushinda michezo mitano, kwenda sare minne na kupoteza michezo miwili.

Mourinho ambaye anakinoa kikosi cha Tottenham amefanikiwa kuingoza timu hiyo kwenye michezo minne ndani ya mwezi Novemba na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo mitatu na kwenda sare mechi mmoja.

Mchezo wa kwanza alifanikiwa kuwafunga Brington kwa mabao 2-1, mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Manchester City pia alifanikiwa kuwafunga mabao 2-1, huku mchezo wa tatu ulikuwa dhidi ya West Brom pia alifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao1-0 na mechi ya mwisho ilikuwa dhidi ya Chelsea ambao walikwenda sare ya bila kufungana.

Mpaka sasa Mourinho amiongoza Tottenham kwenye michezo 11 ya Ligi Kuu nchini England na kuifanya timu hiyo kuwa kileleni kwa pointi 24.

Kwa upande wa kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer aliongoza timu hiyo kucheza michezo minne mwezi novemba ndani ya Ligi Kuu nchini England na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo mitatu na kufungwa mmoja.

Ndani ya mwezi Novemba Manchester United ilipoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwa bao 1-0, na baadae kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Everton, na kufanikiwa tena kuwafunga West Brom bao 1-0, na wakakamilisha michezo ndani ya mwezi huo kwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton.

Solskjaer toka kuanza kwa msimu huu amefanikiwa kuingoza Manchester United kwenye michezo 10 na amefanikiwa kushinda mechi sita huku akipoteza michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja na kukusanya jumla ya alama 19 na kuwa nyuma kwa mchezo mmoja.

Chelsea wao walicheza michezo minne ndani ya mwezi Novemba chini ya Frank Lampard na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili na kwenda sare mchezo mmoja.

Lampard akiiongoza Chelsea mwezi Novemba alikwenda sare dhidi ya Tottenham na kuibuka na ushindi kwenye michezo dhidi ya Sheffield United kwa mabao 4-1, na Newcastle United alipoibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa upande wa David Moyes ambaye ni moja ya kocha mkongwe na wenye uzoefu ndani ya Ligi Kuu nchini England amefanikiwa kuongioza West Ham United kwenye michezo 11 ya ligi kuu na kushinda mechi tano huku akipoteza nne na kwenda sare michezo miwili na kushika nafasi ya nane kwenye msimamo.

Mwezi Novemba Moyes aliongoza West Ham kwenye michezo mitatu na kufanikiwa kushinda michezo yotena kukusanya jumla ya pointi tisa.

Ligi hiyo pia itaendelea mwisho wa juma hili kwa kupigwa michezo mbali mbali huku mpaka sasa Jose Mourinho akiwa juu kwenye msimamo wa Ligi akiwa na Tottenham akifuatiwa na Liverpool wote wakiwa na pointi 24 huku nafasi ya tau ikishikwa na Chelsea yenye pointi 22 na nafasi ya nne wakiwa Leicester City mwenye pointi 21

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!