May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Motsepe Rais mpya CAF

Patrice Motsepe, Rais mpya wa CAF

Spread the love

 

MMILIKI wa klabu ya Mamelod Sundown Patrice Motsepe amechaguliwa kuwa Rais mpya wa shirikisho la mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) akichukua nafasi ya Ahmad Ahmad. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Motsepe amechaguliwa kuwa rais leo tarehe 12 Machi 2021, kwenye mkutano wa 43 wa Caf, uliofanyika jijini Rabat nchini Morocco ambao ulioudhuriwa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) Gian infantino.

Giann Infantino, Rais wa FIFA

Mkutano huo uliodhuliwa na wawaikilishi 54 kutoka kwenye mashirikisho ya mpira wa miguu barani Afrika ambao ndio wapiga kura kwenye uchaguzi huo huku Tanzania ikiwakilishwa na Wallace Karia ambaye ni Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Katika uchaguzi huo Motsepe alikuwa mgombea pekee mara baada ya kukwama kwa rufaa ya Ahmad Ahmad ambaye alitaka kutetea kiti chake mara baada ya kufungiwa kujiusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili.

Ahmad Ahmad aliyekuwa Rais wa CAF

Mara baada aya kutangazwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo Motsepe alimshukuru rais wa Fifa Gian Infantino na kusema kuwa “Tunaweza kutatua changamoto za Afrika kama tukiwa wamoja”

Jina la Motsepe kwenye mpira wa miguu ndani ya bara la Afrika lilianza kuonekana mwaka 2003 alipoinunua timu ya Mamelodi Sundown inayoshiriki Ligi kuu Afrika kusini.

Mamelod Sundown chini ya umiliki wa Motsepe imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Afrika kusini mara tano mfululizo na kushinda taji la Ligi ya mabingwa barani Afrika mwaka 2016.

Licha ya kuwa mmiliki wa Mamelodi Sundown na Rais mpya wa Caf, Motsepe ni tajili namba tisa ndani ya bara la Afrika.

 

error: Content is protected !!