Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Moto wateketeza stoo shule ya Mivumoni Dar
Habari za Siasa

Moto wateketeza stoo shule ya Mivumoni Dar

Spread the love

SEHEMU ya Shule ya Mivumoni Islamic Seminary iliyoko ndani ya Msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeteketea kwa moto, asubuhi ya leo Jumamosi tarehe 18 Julai 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa Mariki Balongo, Mwalimu wa shule hiyo, moto huo ulianza majira ya saa 9:30 asubuhi, katika stoo ya shule hiyo.

Mwalimu huyo amesema, hakuna mwanafunzi aliyeathirika na tukio hilo, bali baadhi ya vifaa vya shule na vya wanafunzi viliteketea kwa moto.

Hata hivyo, Balongo amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

“Ni kweli moto ulitokea sehemu ya stoo ya shule, ulianza saa tatu na nusu asubuhi. Hakuna mwanafunzi aliyedhurika lakini baadhi ya vifaa viliungua,” amesema Balongo.

Amesema moto huo ulidhibitiwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji, kilichofika shuleni hapo saa 10:30 asubuhi.

“Chanzo cha moto hakijulikani nini hadi sasa. Na sidhani kama itakua umeme sababu kwenye hiyo stoo hakuna swichi zaidi ya taa ambayo swichi yake iko nje,” amesema Balongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!