November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Moto wateketeza jengo Coco Beach

Spread the love

JENGO moja katika fukwe ya Coco Beach, limeteketea kwa moto mchana wa leo tarehe 22 Septemba 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jenipher Shirima, Kamanda wa Zimamoto Kinondoni amesema, chanzo cha moto huo bado hakijajukikana.

Shirima ameeleza kuwa, wamepokea taarifa ya moto huo majira ya saa 7.54 mchana, ambapo Jeshi la Zimamoto lilifanikiwa kuudhibiti moto huo.

Hata hivyo, Shirima amesema gari moja la zimamoto limepata ajali njiani likielekea kuzima moto huo.

“Majira ya saa 7.54 tulipokea litokea taarifa ya moto uliowaka kwenye baa maeneo ya Coco Beach, gari yetu ya kwanza iliondoka haraka kwa ajili ya kufika eneo la tukio na walipokea taarifa kwamba moto ni mkubwa inabidi tuongeze nguvu na kwa bahati mbaya wakati gari ya pili inaelekea maeneo hayo ikaanguka,” amesema Shirima.

error: Content is protected !!