
Jengo moja la hostel ya Mabibo likiteketea na moto
MOTO mkubwa umeunguza bweni la Block B la hosteli ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kusababishara hasara ya vitu mbalimbali. Anaandika Pendo Omary…(endelea).
Moto huo ambao chanzo chake hakijulikani ulianza kuwaka katika paa ya moja ya chumba cha ghorofa ya pili ya jengo hilo muda wa saa 4:30 asubuhi leo.
Hasara iliyotokana na moto huo ni kuungua kwa jengo hilo, linalomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kwa sasa halifai kwa matumizi ya binadamu na baadhi ya vifaa vya wanafunzi zikiwemo nguo, vifaa vya kusomea na magodoro.
Aidha wanafunzi walioshuhudia tukio hilo wamelilalamikia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuchelewa kufika katika eneo la ajali.
“Hawa zimamoto tumewatafuta muda mrefu, moto umewaka saa nzima hapa. Tumejitahidi kuokoa baadhi ya mali bila msaada. Wamefika saa moja moto ukiwa tayari umezima. Ni bora tu wasingekuja,” amesema mwanafunzi ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura ambaye alifika katika eneo la ajali amethibitisha kutokea kwa moto huo huku akisema “ bado tunafuatili madhara yaliyopatikana lakini mwanafunzi mmoja ameumia baada ya kuruka kutoka ghorofa ya kwanza wakati akijalibu kujiokoa”
More Stories
Mgomo wa mabasi wanukia Tanzania
NBS yatangaza nafasi za kazi 300
Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania