January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Morsi atupwajela miaka 20

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi

Spread the love

MAHAKAMA nchini Misri, imemhukumu aliyekuwa Rais wa zamani, Mohammed Morsi kifungo cha miaka 20 jela kutokana na mauaji ya waamdamanaji wakati akiwa madarakani. Imeripoti  na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)

Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja ya hukumu zinazomuandama.

Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013, kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.

Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya Ikulu ya Rais mwishoni mwa mwaka 2012.

Wakati umati ulipokusanyika nje ya Ikulu, Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.

Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye makabiliano, wengi kutoka kwa Muslim Brotherhood.

Kabla ya kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa, Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.

error: Content is protected !!