Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Michezo Morrison, Mukoko wafungiwa michezo mitatu
MichezoTangulizi

Morrison, Mukoko wafungiwa michezo mitatu

Bernard Morrison
Spread the love

 

Wachezaji Bernad Morrison wa klabu ya Simba na Mukoko Tonombe kutoka Yanga wamefungiwa kutocheza michezo mitatu na kamati ya mashindano ara baaada ya kufanya makossa ya kinidhamu kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho (ASFC). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo, ulipigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Julai 25, mwaka huu ambapo klabu ya Simba iliibuka kifua mbele kwa kupata ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na kiungo Thadeo Lwanga kwenye dakika ya 79.

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

Katika taarifa iliyotolewa na kamati hiyo jana jioni ilieleza kuwa ilieleza kuwa Morrison alifanya kosa la kimaadili kwa kuvua bukta yake na kubaki na nguo ya ndani mara baada ya mchezo huo kukamilika wakati wa ushangiliaji wa kombe hilo, hivyo atakaa nje kwa michezo mitatu na kulipa faini ya shilingi 3 milioni.

Kwa upande wa kiungo wa Yanga Mukoko amechukuliwa hatua hiyo kufuatia kumipga kiwiko mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco kwenye dakika 45+2, na mwamuzi kumuonesha kadi nyekundu na hivyo kufanya timu yake kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu.

Licha ya Mukoko kufungiwa michezo mitatu lakini pia amepigwa faini ya shilingi 500, 000.

Katika hatua nyingine kamati hiyo ya mashindano pia ilipiga faini ya shilingi 7 milioni, kwa klabu za Simba na Yanga kwa makosa tofauti kwenye mchezo huo.

Klabu ya simba ilipigwa faini ya shilingi 2 milioni kwa kosa la viongozi na baadhi ya mashabiki kukaidi maelekezo kwa kupita kinguvu kwenye mlango usio rasmi wakati wa zoezi la kutembelea uwanja, siku moja kabla ya mchezo.

Aidha pia klabu hiyo ilipigwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la viongozi wa klabu hiyo kutumia mlango wa kubadilishia nguo kuingilia Uwanjani.

Pia klabu hiyo ilipigwa faini nyingine ya shilingi 500,000 mara baada ya mashabiki wao kujiusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kusababisha vurugu na asakari wakati wa mapumziko.

Kwa upande wa klabu ya Yanga kamati hiyo ilianza kwa kuwapiga faini ya shilingi 1,000,000 kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia Uwanjani.

Klabu hiyo pia ilivunja kanuni ya 45:1, kwa baadhi ya watendaji wake na mashabiki kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa mwamuzi wa akiba, hivyo wamepigwa faini ya Shilingi 500,000.

Aidha kiasi kingine ambacho klabu hiyo ilnapaswa kulipa ni shilingi 2 milioni, mara baada ya kupita kwa nguvu mlango usio rasmi wakati wa zoezi la kutembelea uwanja na kufanya uhalibifu.

Pia viongozi wa klabu hiyo wanawajibika kwa kutakiwa kulipa faini ya shilingi 500,000, ara baada ya kutumia mlango wa mashabiki kuingiza timu Uwanjani.

Na faini ya mwisho ilikwenda kwenye klabu hiyo mara baada ya mashabiki wa Yanga kuwarushia chupa za Maji waamuzi wa mchezo huo kinyume na utaratibu na hivyo kutakiwa kulipa kiasi cha shilingi 500,000.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

error: Content is protected !!