August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Morrison aomba radhi Mashabiki Yanga

Spread the love

Mshambuliaji wa kimataifa wa raia wa Ghana Bernard Morison ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu ya Yanga kwa yale yote yaliotokea kipindi alipoondoka klabuni hapo na kujiunga na wapinzani wao Simba. Anaripoti Damas Ndelema

Mchezaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea katika klabu ya Simba aliwaomba radhi mashabiki leo wakati akitambulishwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya mwananchi yaliyofanyika leo Agosti 6 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa

Akizungumza katika tamasha hilo mchezaji huyo alisema anapenda kuwaomba msamaha mashabiki na sasa amerejea nyumbani alisema kuwa miaka kadhaa nyuma aliwahi kusimama katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa na kusema kuwa yupo chuo kikuu ila leo yupo kuchukua elimu ya juu zaidi

“Niliwahi kusisimama hapa na kusema nipo chuo kikuu ila leo nipo hapa kuchukua elimu ya juu masters “

Morisoni ni moja ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga msimu huu na mashabiki wanamatarajio makubwa kutoka kwake hasa kwenye michuano ya kimataifa kwani ni mchezaji mzuri mwenye uzoefu na uwezo mkubwa uwanjani ukiachana na matukio yake ya nje ya uwanja.

error: Content is protected !!