May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Morogoro walilia jiji

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aipandishe hadhi Manispaa ya Morogoro, ili iwe jiji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Shigella ametoa ombi hilo leo Jumatano, tarehe 7 Julai 2021, katika ziara ya kikazi ya Rais Samia, mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro, amesema manispaa hiyo inapendeza kuwa jiji, kwa kuwa iko katikati ya nchi.

Shigella amesema kuwa, wananchi wa Morogoro wameahidi kumchamgua Rais Samia, kama atagombea kiti cha urais wa Tanzania, katika uchaguzi ujao. Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha uongozi wake, ili alifanyie kazi suala hilo.

“Wananchi wameniambia wamejipanga baada ya kipindi cha miaka mitano, utakapogombea mara ya pili, tungependa mansipaa yetu ibadilike iwe Jiji la Morogoro. Ili tuweze kuendana na hadhi ya kuwa katikati,” amesema Shigella.

Kiongozi huyo wa kwanza mwanamke nchini Tanzania, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021 na anatarajiwa kumaliza muhula wake 2025.

Rais Samia huenda akagombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, kama atapitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea.

Rais Samia aliingia madarakani kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Magufuli alifariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Enzi za uhai wake, Magufuli aliipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma, kuwa Jiji, tarehe 26 Aprili 2018. Kwa maelezo kuwa mkoa huo upo katikati ya nchi.

error: Content is protected !!