August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Moro kujenga Hospitali ya Rufaa ya kisasa

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Steven Kebwe

Spread the love

DOKTA Stephen Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amemuagiza Dk. John Ndunguru, Katibu Tawala wa mkoa huo kusimamia uanzishwaji wa mfumo wa kuboresha mapato ya Hospitali ya Rufaa mkoani humo, anaandika Christina Raphael.

Sababu ni kutaka kufanikisha makusanyo ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa itakayokuwa ya kisasa kwenye katika eneo lililotengwa la heka 101 katika Kata ya Tungi, Morogoro.

Dk. Kebwe amesema hayo leo wakati wa sherehe za Siku ya Wauguzi duniani zilizofanyika kimkoa ambapo amemwagiza Katibu Tawala huyo kushirikiana vyema na bodi ya hospitali kuhakikisha mfumo huo unatungwa haraka ili kuweza kukusanya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali na kufanikisha azma hiyo.

Amesema kuwa, tayari eneo la ukubwa wa heka 101 limetengwa katika eneo la Tungi na kwamba, wanatarajia hospitali hiyo kuwa yenye ghorofa saba.

Amesema, ujenzi wa hospitali hiyo unatarajiwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya 700 kwa siku na kwamba, ujenzi huo utaanza mara taratibu za makubaliano baina ya Mkoa na Serikali kukamilika.

Pia Dk. Kebwe amesema, ujenzi huo hautategemea zaidi fedha za ndani bali ni misaada kutoka nchi za Ulaya na kwamba, mpaka sasa wafadhili hao wanatarajia kukabidhi vifaa vya tiba na kinga vyenye thamani ya Sh. 500 milioni.

error: Content is protected !!