July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mongella awatishwa mzigo Ma-DC

Spread the love

JOHN Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amewaagiza wakuu wapya wa wilaya mkoani humo kuhakikisha wanasimamia na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na mauaji ya vikongwe, anaandika Moses Mseti.

Kanda ya Ziwa kwa kipindi kirefu imekuwa ukiandamwa na matukio ya mauaji ya kikatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayohusishwa na imani za kishirikina.

Mongella ametoa agizo hilo leo wakati akiapisha wakuu wapya saba wa Wilaya za Nyamagana, Ilemela, Kwimba, Sengerema, Magu, Misungwi na Ukerewe lililofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mongella amesema kuwa, mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani Mkoa wa Mwanza, kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji hayo.

“Kila mmoja anapaswa kuhakikisha katika wilaya yake, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe, yanatokomezwa, nasema hata kama kucha yake ikipotea hakuna kiongozi atakaelala, tutahakikisha tunaipata kucha hiyo.

“Hiyo ni katika kuhakikisha kila mmoja wetu hapa, suala la ulinzi na usalama linasimamiwa zaidi kwenye kila wilaya husika, hatutakubali kuona DC katika eneo lake ulinzi na usalama ukisuasua kama utasuasua itakuwa moja kwa moja na kazi umeshindwa,” amesema Mongella.

Mongella amesema kuwa, mauaji ya vikongwe na wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakitokea huku viongozi wenye dhamana wakiwemo wakuu wa wilaya wakishindwa kuwashughulikia wahalifu hao.

error: Content is protected !!