Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mongella awakanya watumishi wa umma
Afya

Mongella awakanya watumishi wa umma

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka watumishi wa umma katika idara mbalimbali mkoani humo kuacha kufanya siasa katika sehemu zao za kazi na badala yake waelekeze nguvu zao kuwatumikia wananchi. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mongella amesema kumekuwepo na baadhi ya watumishi wanaofanya siasa mahala pa kazi kwa kuwashawishi watumishi wenzao kuacha kufanya kazi kwa bidii hatua ambayo alidai serikali haita ifumbiwa macho.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh. 20 milioni, iliotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wodi ya akina mama wajawazito (Theater) katika hospitali ya mkoa wa Mwanza.

Alisema kuwa watumishi kazi yao ni kuwatumikia wananchi kwa kufanya kile walichosomea na kwamba masuala ya siasa yana watu wake ambao na wao wameisomea hivyo aliwasisitiza waendelee kuwatumikia wananchi kwa bidii ili kulijenga taifa.

“Watumishi tufanye kazi, tuache siasa na siasa ina watu wake ambao wamesomea, sisi kazi yetu ni kufanya kazi tu naomba tusirudi nyuma na kurudi kule ambako tumetoka,” alisema Mongella.

Pia Mongella aliipongeza benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wadau wakubwa katika masuala ya maendeleo ya mkoa huo kwa kutoa misaada mbalimbali hususani afya kwenye jamii.

Naibu Mkurungezi Mkuu wa Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Joseph Witts alisema michango ya maendeleo wanayoitoa ni kushiriki kuboresha maisha ya watanzania ambao ndio wateja wao wakubwa.

“Tuna mradi mkuu wa kiasi cha Sh. 240 milioni wa kuboresha miundombinu ya jengo la dharura pale Bugando (Hospitali ya Rufaa) na fedha hizo tulizozitoa tumeona zimeleta manufaa na kazi inaendelea kufanyika vizuri,” alisema Witts.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa huo ya Sekou Toure, Dk. Bahati Msaki alisema kiasi cha fedha hizo kilichotolewa na CRDB kitasaidia kuboresha wodi hiyo na kwamba kukamilika kwa wodi hiyo itasaidia kufanyika haraka upasuaji kwa akina mama hao wakati wa kujifungua.

Benki ya CRDB ilitoa msaada wa hudi hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 20 kwenye hospitali ya Sekou Toure pamoja na misaada mbalimbali kwenye hospitali ya rufaa ya Bugando.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika

Spread the loveKATIKA kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba nchini,...

Afya

Ummy Mwalimu:Umeme wa uhakika tija kwa uboreshaji huduma za afya

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na...

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

Afya

Kipindupindu chabisha hodi Dar, wagonjwa 10 waripotiwa

Spread the love  Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka jijini Dar es salaam ambapo...

error: Content is protected !!