August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mongella aanza msako Mwanza

Spread the love

JOHN Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameanza kusaka masalia ya watumishi hewa kwenye Halmashauri ya Jiji hilo, anaandika Moses Mseti.

Katika harakati hizo tayari ameunda kamati ya watu 10 kuchunguza malipo ya watumishi hewa 334 waliobainikwa kwenye uchunguzi wa awali.

Hivi karibuni serikali ilibaini kuwepo kwa watumishi hewa 2, 255 kote nchini ambao wametafuna zaidi ya Sh. 5.5 bilioni huku Mkoa wa Mwanza ukitajwa kuwa kinara kwa kuteketeza zaidi ya Sh.1 bilioni.

Jana Mongella amesema kuwa, idadi ya watumishi hewa 334 inaweza kuongezeka zaidi hivyo bado wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini idadi nyingine ya watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma bila kuzitolea jasho.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, pamoja na mengine aliwahimiza wanahabari kuendelea kufichua madudu yanayofanywa katika taasisi mbalimbali nchini.

Amesema kuwa, katika Halmashauli ya Jiji la Mwanza kuna watumishi hewa wengi hususani walimu ambao alidai kuwa baada ya kupata kazi na siku ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi, huondoka bila taarifa huku malipo yakiendelea kufanyika.

Amesema, wameamua wameunda tume ya watu 10 kutoka katika ofisi yake, kupiga kambi ya siku wiki moja katika jiji hilo ili kuchunguza malipo ya watumishi hao yalivyokuwa yakifanyika.

Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo amesema, uchunguzi uliofanywa umbebaini kuwa watumishi hao walikuwa wakilipwa mishahara kwa madai kwamba ni wagonjwa na wengine wapo masomoni.

“Watumishi wengi walikuwa wanalipwa mshahara kwa madai wapo masomoni, wengine wakiwa ni watoro, wagonjwa na wanaendelea kulipwa kwa kisingizio hicho lakini hakuna taarifa inayodhibitisha jambo hilo,” amesema.

Amesema ni kitendo cha kusikitisha, cha kushangaza na kwamba ni wizi wa mchana kwa wakuu wa idara hususani kitengo cha elimu kuendelea kuwalipa watumishi ambao hawapo kazi huku akidai kitendo hicho hakitafumbiwa macho.

error: Content is protected !!