May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Monalisa awa msemaji wa Simba Queen

Spread the love

 

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam nchini Tanzania, imemtangaza muigizaji maarufu nchini humo,
Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ kuwa msemaji wa timu ya wanawake ‘Simba Queens.’ Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kuraza za kijamii za Simba, leo Jumatano tarehe 3 Machi 2021, zimeweka picha ya Monanisa akitambulishwa na mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji, akimkabidhi jezi.

“Mlezi wetu Fatema Dewji, amemkaribisha rasmi Monalisa, kama msemaji wa Simba Queens. tunaimani Monalisa atafanya kazi nzuri katika kueneza taarifa zote zinazohusiana na Simba Queens kwenye jamii yetu.”

“Kwa uzoefu wa Monalisa, tunaimani atakwenda kuwa msemaji bora wa timu yetu na uzoefu wake aliokua nao katika jamii. Karibu Simba Queens Msemaji Wetu, Monalisa.” Imeeleza Simba kwenye maneno yaliyoambana na picha hizo za utambulisho.

Naye Monalisa amezungumzia nafasi hiyo mpya kwenye medani za soka kupitia akaunti zake za kijamii akisema “mimi ni Simba Jike. Simba Queen”

“Sisi ni Simba twacheza Rumba Tanzania. Natamani kumalizia wimbo huu adhimu wa kuisifia nchi yangu lakini natamani mjue furaha yangu. Ahsante Mungu, Ahsante Wanasimba wote na mwisho Ahsante mama mlezi wa Simba Queens Fatema Dewji kwa kunikabidhi kijiti cha kuisemea timu yangu pendwa ya Simba Queen,” amesema Monalisa

“Sasa ni muda wa kazi, muda wa kuionesha dunia ukubwa wa Simba, huko mlipo furahini na mfurahi haswa. Mwisho, naomba kutoa tangazo rasmi ya kwamba kila binti/mwanamke nchi hii ni shabiki wa Simba Queens.”

Monalisa amemalizia akisema “nichagulieni jina la kazi.”

error: Content is protected !!