October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mojonzi yaikumba Sierra Leone.

Spread the love

MIILI ya watu takribani 400 nchini Sierra Leone katika eneo la Regent na maeneo ya jirani mjini Freetown inatarajiwa kuzikwa leo katika mazishi ya pamoja kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo, anaandika Irene David.

Msemaji Mkuu wa Rais, Abdulai Baraytay, ametoa kuwa mpaka sasa miili ya watu 600 imetoweka kutokana na kufukiwa kwa matope na vufusi ukujitiada zikiendelea kuwaokoa walioniusurika na maporomoko hayo.

“Jamii nzima inaomboleza, wapendwa wengine wametoweka, takribani miili ya watu 600 imetoweka,” amesema Abdulai.

Abdulai amesema shughuli za mazishi kwa miili 400 waliofariki kufuatia maporomoko hayo yatafanyika leo ili kupunguza idadi ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Aidha Umoja wa Mataifa (UN) umesema wafanyakazi wake waliopo nchini humo wanaendelea kufanya jitiada za kuiokoa miili mingine na walionusurika.

error: Content is protected !!